BIBLEPAGE.NET

Someni Neno la Mungu juu ya Internet

Aya ya Siku

Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia

Mithali 13:20


 

Sura ya 51Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.
2Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu);
3wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.
4Wana wa Yoeli; mwanawe huyo ni Shemaya, na mwanawe huyo ni Gogu, na mwanawe huyo ni Shimei;
5na mwanawe huyo ni Mika, na mwanawe huyo ni Reaya, na mwanawe huyo ni Baali;
6na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.
7Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria,
8na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni;
9na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
10Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
11Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka;
12Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani;
13na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba.
14Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi;
15Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao.
16Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake.
17Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli.
18Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani.
19Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu.
20Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.
21Wakateka nyara ng'ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu.
22Kwani wengi walianguka waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa badala yao hata wakati wa ule uhamisho.
23Na wana wa nusu-kabila ya Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni.
24Na hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao; Eferi, na Ishi, na Elieli, na Azrieli, na Yeremia, na Hodavia, na Yadieli; watu hodari wa vita, watu mashuhuri, wakuu wa mbari za baba zao.
25Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao.
26Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru na roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo. • Matoleo mengine  
 • English
 • Français
 • Deutsch
 • Español
 • Português
 • Italiano
 • Nederlands
 • Român
 • Dansk
 • Svensk
 • Suomi
 • Norsk
 • Čeština
 • русский
 • Український
 • Български
 • Polski
 • Hrvatski
 • Magyar
 • Shqiptar
 • Türk
 • עברית
 • 圣经
 • 聖經
 • 한국의
 • 日本語
 • Tiêng Viêt
 • ภาษาไทย
 • Tagalog
 • Indonesia
 • हिन्दी
 • தமிழ்
 • ਪੰਜਾਬੀ
 • اردو
 • Somali
 • Kiswahili
 • العربية